This site is being Upgraded

Care is Our Duty

Governance

USHIRIKI WA RAIA KATIKA KUONGEZA UTAWALA BORA KWENYE MASUALA YA LISHE KATIKA WILAYA ZA MULEBA, BAGAMOYO NA MASASI

 Utangulizi


Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya za Bagamoyo, Muleba na Masasi ina mpango wa kuzijingea uwezo Asasi za Kiraia ili kuziwezesha kushirikiana na Halmashauri hizo za wilaya katika kuboresha lishe ya wananchi wao. Ushiriki wa Asasi za Kiraia katika kupanga na kuandaa bajeti ya lishe unatarajiwa kuboresha utengaji wa rasilimali kwa masuala yanayowahusu watu wenye kipato cha chini sana. Hivyo basi, Asasi za Kiraia zinatakiwa kuwa washirika wa kimkakati wa Halmashauri za wilaya katika kupanga, kuandaa bajeti na utekelezaji wa mipango ya lishe. Hii itafanikiwa kupitia mradi wa miaka mitatu ‘‘Lishe Wajibu’’ unaofadhiliwa na Foundation for Civil Society kuanzia Januari 2015 hadi Disemba 2017.

Mradi wa Lishe Wajibu unalenga kuzijengea uwezo Asasi za Kiraia katika kuharakisha utekelezaji wa shughuli za lishe kupitia utawala bora ili

 kupunguza udumavu wa utotoni kwa asilimia 2 kutoka hali ilivyo sasa kwa miaka 3 katika wilaya tatu za mradi. Wilaya hizo ni Muleba (Kagera), Masasi (Mtwara) na Bagamoyo (Pwani).

Utawala bora ni ule unaowezesha umiliki sahihi wa rasilimali na kukidhi mahitaji ya msingi ya raia wake na hivyo kuiwezesha jamii kuwa na msingi wa haki na usawa. Nguzo tatu za utawala bora ni uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji. Uwajibikaji unapaswa kuangalia utoaji huduma pamoja na mahitaji ya raia ili kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu zikiwepo za afya na lishe kwa jamii nzima.

Hali ya sasa ya Lishe katika mikoa ya Kagera, Mtwara na Pwani


Jedwali 1, linaonesha hali ya lishe kwa wajawazito na watoto chini ya miaka 5 katika mikoa ya mradi pamoja na hali ya kilishe kitaifa kupitia taarifa kutoka TDHS 2010 na utafiti uliofanywa na Taasisi cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC 2014).

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these